Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za sekta ya utalii ikiwemo ajira, kuuza mazao wanayozalishwa nchini na usafirishaji.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua Mkutano wa pili wa Kimataifa wa sekta ya utalii na Maonesho “The Z Summit 2024” katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar.
Amesema, Serikali itaendelea kujenga miundombinu ya ujenzi wa barabara mpya, kuboresha usambazaji wa umeme na maji pamoja na viwanja vya ndege.
Rais Mwinyi ameongeza kuwa Sheria mpya ya uwekezaji Zanzibar ya mwaka 2024 imeweka vivutio vingi ambavyo vinalinda uwekezaji na kuwa vivutio vya kodi Afrika Mashariki.
Aidha, amesema Pemba ni chachu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya baadae kwa kuanzishwa ukanda wa uwekezaji wa Pemba (PIZ) ili kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za kiuchumi.