Mabingwa wa Soka Barani Afrika Klabu ya Al Ahly ya Misri wameomba mchezo wao wa Mzunguuko watano wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Madeama usogezwe mbele.

Mchezo huo ambao unapaswa kucheza nchini Ghana, umepangwa kuchezwa kesho Ijumaa (Februari 23) na sasa Al Ahly wameomba   uchezwe keshokutwa Jumamosi (Februari 24).

Sababu kubwa iliyowasilishwa CAF na miamba hiyo ya Soka Barani Afrika ni kufuatia usafiri wao wa ndege kupata itilafu wakiwa uwanja wa ndege wa International airport Accra na kushindwa kwenda Kumasi ambako mchezo utachezwa.

Kwenye maelezo ya Al Ahly waliyotoa kwenda CAF, wamedai kuwa wakiwa mjini Accra jana Jumatano (Februari 21) ndege yao ilipata hitilafu, hivyo hawakupata usafiri mwingine wa kuwafikisha Kumasi kwa wakati.

Mgongano wa tumbo na sehemu ya mbele ya ndege ulisababisha hitilafu, na kuifanya timu hiyo ya Misri kushindwa kuendelea na safari ya kwenda Kumasi.

May be an image of text

Licha ya jitihada za kupata ndege mbadala ya ndani, timu ya Al Ahly illazimika kulala mjini Accra, na hivyo kukwamisha mipango yao ya kuwasili na kufanya maandalizi kwa wakati.

Kwa mujibu wa kanuni za Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly wanatakiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa mechi siku ya leo Alhamisi (Februari 22), kazi ambayo kwa sasa inatatizwa na hali isiyotarajiwa.

Kwa kuzingatia itifaki za Michuano ya CAF, Al Ahly wamewasiliana na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF, wakitaka kuahirishwa kwa siku moja kwa mechi iliyopangwa kwenye Uwanja wa Baba Yara siku ya ljumaa.

Hata hivyo Klabu hiyo inasubiri majibu kutoka CAF ili kukabiliana na changamoto zisizotarajiwa ambazo wamekutana nazo katika safari ya kwenda kukabiliana na Medeama.

Mripoti kwa kina mapungufu sheria za Habari - Dkt. Mzuri
Greenwood aipagawisha FC Barcelona