Hali ya uchumi ya FC Barcelona inatoka kwenye afadhali na kuwa mbaya zaidi baada ya La Liga kuiambia klabu hiyo kuuza mastaa wake ili kupunguza bili ya Pauni 57 milioni kwenye mishahara.

Miamba hiyo ya Nou Camp mambo yao si matamu sana kwenye ligi msimu huu, ikishika nafasi ya tatu, nyuma ya Girona kwa tofauti ya alama mbili na mahasimu wao Real Madrid kwa tofauti ya alama nane.

Lakini, pengo hilo linaweza kuwa kubwa zaidi miaka michache inayokuja kutokana na hali ya uchumi wa Barcelona kuzidi kudorora jambo litakalowafanya kushindwa kuwa na wachezaji wa maana kikosini.

La Liga ilitangaza kwamba Barcelona inapaswa kushusha bili yake ya mishahara kutoka Pauni 231 milioni hadi Pauni 174 milioni kwa ajili ya msimu ujao wa 2024/25.

Jambo hilo litaifanya ilazimike kuwapiga bei baadhi ya wachezaji wake ili kuendana na hitaji la La Liga juu ya usawa kwenye mapato na matumizi ya kikosi hicho.

Kocha, Xavi Hernandez alitangaza kwamba mwishoni mwa msimu huu atang’atuka na kuachana na timu hiyo ya Nou Camp.

Na sasa majina makubwa ambavo yamekuwa yakihusishwa na mpango wa kufunguliwa mlango huko Nou Camp ni pamoja na Frenkie de Jong, ambaye mshahara wake ni mkubwa sana, Robert Lewandowski, Gavi, Raphinha, Ronald Araujo na Pedri.

De Jong amerejea tena kwenye rada za Manchester United baada ya kuwindwa misimu miwili iliyopita tangu kocha Erik ten Hag alipojiunga na miamba hiyo ya Old Trafford. Na sasa, kiungo huyo wa Kidachi mwenye miaka 26 anaweza kufungua milango ya kwenda kukipiga Old Trafford.

Sir Jim Ratclife hana baya
Gaucho anasubiri muda Zambia