Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini England Jude Bellingham, anajiandaa kubadilishiwa nafasi ya kucheza ndani ya uwanja, ili kutoa nafasi ya Kylian Mbappe kufiti kwenye kikosi cha Real Madrid.

Mshambuliaji huyo wa Ufaransa, Mbappe anaripotiwa kukubali mkataba wa miaka mitano huko Bernabeu ambako atajiunga bure mwishoni mwa msimu huu, dili lake litakapofika tamati huko PSG.

Mbappe mwenye umri wa miaka 25, alimwambia rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi uamuzi wake wa kuhama Jumnanne, Juma lililopita iliyopita.

Licha ya kwamba hakuna karatasi zozote rasmi zilizosainiwa, Real Madrid imejiweka tayari kabisa kwa ajili ya kumpokea kwenye kikosi chao, hiyo ikiwamo atafiti wapi kwenye timu hiyo ya mastaa watupu inayonolewa na Mtaliano, Carlo Ancelotti.

Ripoti zinadai kwamba Los Blancos imepanga kumtumia Mbappe kwenye nafasi yake pendwa, upande wa kushoto, kuliko kutumika kama Namba 9.

Eneo hilo kwa sasa anacheza Vinicius Junior ili kumruhusu Bellingham kucheza Namba 10 au wakati mwingine kama Namba 9 bandia.

Lakini, sasa mmoja kati ya Bellingham na Vinicius watalazimika kubadilisha nafasi zao za uwanjani kumfanya Mbappe kucheza kwenye upande wa kushoto, ambao amekuwa akitoa huduma bora kabisa uwanjani.

Eneo ambalo Bellingham amekuwa akicheza limempa mafanikio makubwa baada ya kufunga mabao 20 na asisti nane katika mechi 29, lakini sasa atalazimika kushuka chini na huenda akacheza Namba l0, ili pale kwenye Namba 9 bandia apangwe Rodrygo.

Mbappe atakwenda Real Madrid ikifahamika wazi uwezo wake wa kufunga mabao, ambapo huko kwenye kikosi cha PSG ametikisa nyavu mara 244 katika mechi 291 na hivyo kuwa mfungaji mahiri PSG.

Gaucho anasubiri muda Zambia
Mangalo, Kagoma waivuruga Singida FG