Lydia Mollel – Morogoro.
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia Mwanaume Mmoja (30(, Mkazi wa eneo la Mafisa lililopo Manisapaa ya Morogoro, kwa tuhuma za kumbaka binti yake wakumzaa mwenye umri wa miaka mitatu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema taratibu za kisheria zinakamilishwa ili kumfikisha mtuhumiwa Mahakamani.
Katika hatua nyingine SACP Mkama, ametoa wito kwa Wazazi/Walezi kuweka ulinzi kwa watoto, ili kuepuna na vitendo vya kikatili dhidi yao.
Hata hivyo, wakizungumza na Dar24 Media kwa nyakati tofauti, baadhi ya Walezi na Viongozi wamesema kubainika kwa kitendo hicho kimefanikishwa na Mwalimu wa mtoto huyo ambapo aliona utofauti wa kutembea na baadae alimfikisha hospitali ili kujiridhisha.
Wamsema, badae kwa kushirikiana na Viongozi wa Mtaa, Afisa ustawi wa jamii wakaazimia kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa kwenye mikono ya sheria .
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa kushiriakiana na Polisi Kata pamoja na Dawati la Jinsia wamekuwa wakitoa elimu maeneo tofauti, ili kuhakikisha Matukio ya kiuhalifu yanatokomezwa.