Tajiri wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe, ameweka wazi kwamba bado hakuna uhakika kama mastaa wa timu hivo, Mason Greewood na Jadon Sancho watarudi kwenve kikosi kwa msimu ujao, ama ndio itakuwa mwisho wao.
Greenwood, ambaye alienda Getafe ya Hispania Septemba mwaka jana kwa mkopo wa msimu mmoja ikiwa ni baada ya kutokutwa na hatia juu ya tuhuma za unyanyasaji wa kijinsi zilizokuwa zinamkabili, msimu huu ameonyesha kiwango bora akiwa na Getafe.
Licha ya kutokutwa na hatia juu ya mashtaka yaliyokuwa yanamkabili, Man United ilishindwa kumrudisha kikosini staa huyo kutokana na pingamizi Iililowekwa na baadhi ya wafanyakazi na wachezaji wa kike.
Sancho kwa sasa yupo zake Borussia Dortmund kwa mkopo wa nusu msimu baada ya kuingia kwenye mgogoro na kocha wake Erik ten Hag aliyetupiana naye maneno kupitia mitandao ya kijamii, hali iliyosababisha ashushwe kwenda kikosi cha vijana Septemba mwaka jana kabla ya kutolewa kwa mkopo Januari mwaka huu.
Tajiri Ratcliffe amesisitiza kwamba wanachoendelea kuangalia ni kanuni ikiwa zinaruhusu kuwarudisha au laa, na sio jina la mchezaji.
Tutafanya uamuzi, sijajua kama Greenwood ataendelea kuwa hapa ama ataondoka, kitu ambacho naweza kusema kwa sasa ni kanuni ndio zitaenda kufanya uamuzi, je ni mchezaji mzuri tunayemhitaji? Je, tunafurahia uwepo wake? Je, ana tabia nzuri nje ya uwanja. Kwa hiyo jibu ni jepesi”