Zanzibar imetajwa kuwa mwenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa mwaka 2024 ‘CECAFA Senior Challenge Cup 2024’.

Maamuzi hayo yamefikiwa kwenye Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ uliofanyika leo Ijumaa (Februari 23) mjini Mombasa nchini Kenya.

Kikao hicho pia kimefikia maamuzi ya kuipa Zanzibar kuwa mwenyeji wa Michuano ya Shule ‘CAF School Football Championship’.

Uganda itakuwa wenyeji wa Michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chici ya umri wa miaka 17 katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ‘AFCON U-17 Boys CECAFA Zonal’, huku Tanzania ikitajwa kuwa mwenyeji wa Michezo ya Afrika chini ya miaka 20 ‘AFCON U-20 CECAFA Zonal’.

Nayo nchi ya Ethiopia imepewa uenyeji wa Michezo ya Kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Afrika MAshariki na Kati kwa Wanawake ‘CAF CECAFA’ na michuano ya CECAFA ya Wanawake chini ya Miaka 20 ‘CECAFA U-20’.

Young Africans kuibadilikia CR Belouizdad
DCEA yahitimisha mafunzo kwa Maafisa waelimishaji wa TAKUKURU