Afarah Suleiman, Babati – Manyara. 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Manyara, SACP George Katabazi leo februari 22, 2024 ametoa jumla ya kadi 42 za Bima ya afya kwa Kaya saba zenye mahitaji maalum wakiwemo, watu wenye ulemavi na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Akikabidhi kadi hizo za Bima hizo, Kamanda Katabazi amesema kadi hizo za bima zitaweza kuwasaidia wanufaika kimatibabu katika hospitali zote za Serikali.

Amesema, waliona kuna haja ya kutoa kadi za bima kutokana na baadhi ya kaya kushindwa kumudu gharama za matibabu kwa kuwa na hali ngumu za kiuchumi walizonazo, hivyo kiendo hicho pia kitadumisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii.

Wakitoa neno la shukran, baadhi ya wanufaika wa kadi hizo za bima ya afya wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuona na kuamua kuwasaidia, kwani walishindwa kumudu gharama za matibabu kutokana na hali walizonazo kiuchumi.

Nahodha Tabora Utd aitangazia vita Singida FG
Wanane mbaroni kwa tuhuma za mauaji