Pamoja na uwepo wa tetesi za Karim Benzema kutaka kuondoka Saudi Arabia, mchezaji huyo amevunja ukimya na kusema hana mpango wa kuondoka Al-Ittihad.

Benzema aliyejiunga na Al-Ittihad msimu uliopita, kwa mkataba wa miaka mitatu, akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika Real Madrid, amekuwa akihusishwa kutaka kuondoka Saudi Arabia kwa kuwa hana maelewano na Kocha Marcelo Gallardo.

Hata hivyo, Benzema amekanusha tetesi hizo na kusema hana tatizo lolote na Gallardo na anafurahia maisha ya Saudi Arabia.

“Nimerejea nikiwa na kiwango bora zaidi, sina tatizo na mtu, mnaweza kumuuliza kocha kama ana ugomvi na mimi, puuzeni uzushi kwani nina furaha nikiwa hapa,” amesema

“Maisha yangu kwa sasa yapo Saudi Arabia, sina mpango wa kurudi kucheza Ulaya, nitakuwa hapa hadi nitakapomaliza mkataba wangu.”

Awali, ilielezwa kuwa, Benzema alikasirika baada ya kuondolewa katika kikosi cha kwanza baada ya kuchelewa kutoka katika Kutokana na hali hiyo, mchezaji huyo hakusafiri na wenzake timu ilipokwenda kambini Dubai.

Pia, Benzema alitemwa katika kikosi kilichokwenda Navbahor Namangan, Uzbekistan kujiandaa na michuano ya Bara la Asia.

De Bruyne kung'oka kwa Pauni Milioni 100
Benchikha aahidi makubwa Ligi ya Mabingwa