Beki kutoka nchini Ufaransa na, Raphael Varane ndiye anayelengwa zaidi nchini Saudi Arabia katika uhamisho wa majira haya ya joto huku Al Ittihad na Al Nassr zikishindana kutoa ofa kwa sasa.
Mkataba wa Varane katika kikosi cha Man Utd unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2023/24, ingawa klabu hiyo haijakataa kuongezwa kwa masharti yaliyopunguzwa, sawa na majaribio ya mwisho ya msimu wa joto ambayo hayakufaulu kumbakisha David de Gea.
Beki huyo ana matumaini ya kuepuka hali kama hii, ambapo haikufahamika iwapo Mlinda Lango huyo kutoka nchini Hispania angepokea ofa ya mkataba mpya baada ya mkataba wake wa awali kumalizika.
Maslahi ya Varane yataongezeka kama ataelekea Saudia, kwani Al Ittihad inatayarisha ofa yenye thamani ya karibu euro milioni 30 kwa msimu, na fursa zingine za mapato zaidi.
Tayari wameshawasiliana kwa maneno na kambi ya Varane kuelezea ofa yao.
Al Shabab pia wamemjadili Varane, lakini itakuwa vigumu kwa klabu isiyodhibitiwa na PIF kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
PIF wana hisa za kuidhibiti Al Ittihad, Al Nassr, Al Ahli na AI Hilal.
Al Ittihad na AI Nassr wanatumaini kumpata Varane kwa mkataba wa miaka mitatu iwapo wataendelea na majaribio ya kumsajili.
Kama ilivyo kwa N’Golo Kante kwenda Al ittihad, wafanyabiashara wa kati huenda wakaamua klabu ya mwisho ambayo atatua.