Johansen Buberwa – Kagera.
Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Taifa inayoongozwa na Mwenyekiti wake na Mjumbe wa Kamati kuu, Fadhir Rajab Maganya inatarajiwa kufanya ziara ya siku tano mkoani Kagera, kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi – CCM.
Akizungumza na Vyombo vya Habari hii leo Februari 26, 2024 Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama hicho Mkoa wa Kagera, Hamim Mahmoudu amesema ziara hiyo inatarajiwa kuanza Machi 4, 2024 ambapo ikiwashirikisha Mwenyekiti, Makamu wake pamoja na Wajumbe wa kamati ya utekelezaji Taifa.
Katika ziara hiyo, yatagawanywa makundi mawili ili kuleta ufanisi ambapo la kwanza litaongozwa na Mwenyekiti kwenda katika Wilaya za Biharamulo, Ngara, Kyerwa, Karagwe na Bukoba Manispaa.
Kundi jingine litaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa wakitembelea Wilaya za Muleba, Bukoba Vijijini na Missenyi kisha wote kukutana na kufanya majumisho Machi nane mwaka huu katika Manispaa ya Bukoba.