Licha ya kusifiwa kwa kiwango alichoonyesha kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle, Bukayo Saka amejibu maneno mawili tu alipoulizwa juu ya kiwango chake.

Katika mchezo huo ambao Arsenal iliibuka na ushindi wa mabao 4-1, Saka ilifunga bao moja dakika ya 65 na kuzidi kuisogeza Arsenal kwenye mazingira mazuri ya kuwania taji la Ligi Kuu England msimu huu 2023/24.

Saka alionyesha kiwango bora kwenye mchezo huo ikiwa ni siku kadhaa tangu beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand kudai staa huyo hana viwango vya dunia.

Alipofanyiwa mahojiano na mtangazaji wa kituo cha TNT Sports Jules Breach baada ya mechi akiwa na Kai Havertz, Saka alisema hana maoni juu ya bao alilofunga licha ya mtangazaji kumwambia linaweza kuwa bao la viwango vya dunia.

Saka amezidi kung’ara ikiwa ni wiki chache tangu aweke rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza mdogo zaidi wa Arsenal kuwahi kufikisha mabao 50 ya Ligi Kuu England.

Hata hivyo, Ferdinand haamini juu ya ubora wake akisisitiza staa huyu bado hajaonyesha kiwango bora kwenye michuano mbalimbali kama Ligi ya Mabingwa ingawa anaamini bado ni mchezaji bora.

Mambo mazuri yanukia Old Trafford
Martin Odegaard: Tunaishi katika ndoto