Meneja Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally anaamini mafanikio ya Young Africans katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, yamechagizwa na uwekezaji wa Mohamed Dewji ‘Mo’.

Young Africans juzi Jumamosi (Februari 23) ilitinga Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25, ikiifunga CR Belouizdad mabao 4-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Ahmed Ally ameweka wazi imani yake hiyo, alipozungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Jumatatu (Februari 26), alipozungumzia maandalizi ya mchezo wao wa mwisho wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Ahmed Ally amesema: “Kufuzu kwa Young Africans katika hatua ya Robo Fainali wa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba ni Mohammed Dewji na wa pili ni Simba SC.

Wakati Mo anakuja kuwekeza Simba alisema vision yake ni kushinda ubingwa wa Afrika na baada ya hapo tukaanza mchakato wa kutawala soka la Afrika.

Wakati Mohammed Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua.

Baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri. Kama Simba SC na Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira, malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi. Huu ndio ukweli ambao utadumu milele.”

Benchikha awataka Jwaneng Galaxy
Tshabalala: Kazi tutaimaliza nyumbani