Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Kutokana na matukio mengi ya mauwaji ya Madereva wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda ndani ya kipindi kifupi, Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, ASP Amiri Mlemba ametembelea vijiwe vya bodaboda na kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na abiria wahalifu.

Mlemba ameamua kutembelea vijiwe hivyo ili kuwaelimisha na kuwaeleza kwamba Polisi itaendelea kufanya Wilaya nzima, ili kuhakikisha mauji hayo yanadhibitiwa na kumalizika kabisa.

Kwa upande wao baadhi ya Madereva Bodaboda wameliomba Jeshi la Polisi kufanya msako wa Pikipiki zote ambazo hazina namba za usajili ili zikamatwe, kwani wanahisi  zinakuwa chanzo cha uhalifu wa matukio mbalimbali.

Kidunda: Asemahle Wellem hatanisahau
Wanawake watakiwa kuzipambania ndoto zao