Mabondia wa Ngumi za Kulipwa nchini Tanzania, Mada Maugo na Karim Mandonga, wanatarajiwa kumaliza ubishi wa nani zaidi kwenye pambano litakalofanyika mapema Aprili mwaka huu, jijini Dar es salaam.

Mabondia hao watapanda ulingoni kwenye pambano la raundi 6 na kilo 79.

Maugo amesema anataka kutoa burudani kwa mashabiki wake baada ya kukaa muda mrefu bila kupigana, kwani anaamini Mandonga hamuwezi.

“Nitamfundisha adabu Mandonga katika pambano hilo, hajawahi kupigwa alikuwa anaguswa guswa kwenye mapambano aliyocheza, nitampasua ili ajue mimi ni nani,” amesema Maugo

Bondia huyo amesema anasubiri tarehe ya pambano hilo mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo ya waandaaji pamoja na wadhamini.

Kocha wa Maugo, Mmarekani Seko Tongola, amesema amekuja hapa nchini kwa ajili ya kumsimamia bondia wake huyo.

“Leo, nitaanza kumpa mbinu bondia wangu zitakazomsaidia kufanya vizuri kwenye pambano hilo kwa kuwa hajapigana muda mrefu, ninapaswa kumpa mazoezi ya nguvu ili aimarishe mwili wake kabla ya kukutana na mpinzani wake,” amesema Tongola.

Amesema kabla hajawasili alikuwa anamfundisha kwa njia ya video akiwa nchini Marekani, lengo likiwa ni kuhakikisha Ushindi unapatikana.

Luis Enrique: Tunatakiwa kubadilika bila Mbappe
Antony kuondoka Old Trafford