Mshambuliaji wa Mashujaa FC, Reliant Lusajo ametamba kuifungia timu hiyo mabao mengi kuliko alivyokuwa Namungo FC.

Mshambuliaji huyo amesema hiyo ni kutokana na uwepo wa viungo wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi.

“Kazi yangu ni kufunga na ninaamini nitafunga mabao mengi sana nikiwa hapa Mashujaa FC, kwa sababu tuna viungo wenye uwezo wa kufunga lakini pia kutengeneza nafasi, hatua ya kuaminiwa na kocha inanipa urahisi kufanya hivyo,” amesema Lusajo.

Mchezaji huyo amesema mbali na uwepo wa viungo wengi wa kutengeneza nafasi lakini anaushirikiano mzuri na mshambuliaji mwenzake Adam Adam, hivyo hilo ni moja ya jambo ambalo linampa nguvu ya kuendeleza kile alichokifanya akiwa Namungo.

Amesema lengo lake yeye na mwenzake ni kuipigania timu hiyo kuondoka nafasi mbaya iliyopo hivi sasa, na kukaa nafasi za juu ili kuendelea kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Lusajo aliyejiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo tayari ameifungia Mashujaa FC mabao mawili katika michezo minne iliyopita.

Polisi yawaonya wanaojichukulia sheria mkononi
Ley Matampi afichua siri ya mafanikio