Boniface Gideon – Tanga.

Kanisa la Mennonite Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Huduma yangu Furaha yangu (HYFY), wametoa msaada wa ufadhili wa vifaa kwa wanafunzi 16 wa shule za Awali, Msingi na Sekondari, ikiwemo mabinti walikatisha masomo baada ya kupata ujauzito.

Akizungumza katika Kanisa la Mennonite lililopo  Pongwe wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya Elimu zikiwemo Sare za Shule, madaftari, kalamu na viatu, Meneja mipango kutoka Shirika hilo , Magesa Wambura alisema mpaka sasa wameshawafikia Wanafunzi zaidi ya 200 wanaotoka kwenye mazingira magumu na kuwasaidia misaada mbalimbali ili waendelee na masomo yao.

Amesema, “moja ya chanzo kikubwa cha watoto kukatisha masomo ni pamoja na umasikini ambao husababisha Mabinti kupata ujauzito kwakudanganywa na vitu vidogo vidogo pamoja , huku sababu nyengine kubwa ikiwa ni Wazazi kushindwa kutimiza wajibu wao.”

Aidha, Wambura ameongeza kuwa, “Yapo mambo mengi yanayoweza kumfanya mtoto ashindwe kuendelea na masomo yake na kutimiza ndoto zake alizojiwekea, lakini kubwa zaidi ni Umasikini pamoja na wazazi kushindwa kutimiza wajibu wao, haya ndio mambo makubwa yanayosababisha mwanafunzi kushindwa kuendelea na masomo.”

Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa la Mennonite Pongwe, Naftali Magai alisema huo ni mpango kazi wa Kanisa hilo katika kuhakikisha Watoto wanatimiza ndoto zao na kwamba watoto wote wanaoingia kwenye ufadhiri huo watafadhiriwa kupata Elimu kuanzia ile ya awali hadi chuo kikuu,

Aliwashukuru wadau hao kwa kutoa ufadhili wadau hao wa elimu ambapo amewasisitiza wazazi kuzingatia umuhimu wa elimu pamoja na malezi ya kidini ili kuweza kujenga jamii iliyobora kwa maslahi mapana ya kizazi cha baadaye.

“Mafundisho ya kiimani na elimu ya shule ni vitu vya msingi sana na vyakutegemea kwa wazazi ili watoto wetu tuweze kuwalea katika malezi bora hii itasaidia sana kujenga kizazi cha jamii ya maadaye endapo watapata elimu pamoja na kuwa na hofu ya Mungu” Alisema Magai.

Watatu wafanyiwa upandikizaji wa betri kwenye Moyo BMH
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 29, 2024