Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ametaja sababu 10 za Dkt. Samia Suluhu Hassan Kustahili Kuwa Rais qa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania mpaka 2030.

1. RAIS SAMIA ANA MAONO YA KUWAUNGANISHA WATANZANIA

“Uliapishwa kuwa kiongozi wetu Machi 19, 2021. Na uliingia katika mazingira magumu ambayo hayajawahi kutokea katika nchi yetu. Mazingira ya msiba ambao uliwachanganya Watanzania wengi baada ya Rais wao, kipenzi chao aliondoka.

Haijawahi kutokea katika Historia ya nchi yetu. Na wewe ukaapishwa siku mbili baada ya kutangaza msiba ule. Hakikuwa kipindi rahisi. Ilihitaji mfariji kuwafariji Watanzania katika kipindi hiki kigumu ambacho walikuwa wamechanganyikiwa.

Ilihitaji kauli za matumaini na vitendo vya matumaini. Ilihitaji maono ya kuwaunganisha Watanzania katika kipindi hiki. Mheshimiwa Rais, nchi yetu ilihitaji mfariji na wewe ulikuwa mfariji katika kipindi hiki kigumu.

Hilo peke yake hata usipochanganya na mambo mengine yoyote ambayo umeyafanya unastahili kuwa kiongozi wetu mpaka mwaka 2030,” January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

2. UJASIRI WA KUINGIZA CHANJO YA UVIKO UNAKUPA SIFA UENDELEE KUWA KIONGOZI WETU

“Mheshimiwa Rais vile vile uliingia madarakani katika kipindi ambacho kuna mambo yalikuwa yamepangwa na kiongozi aliyepita. Na yalikuwa yameamuliwa na yametolewa uamuzi. Lakini wote tunajua yalihitaji mabadiliko.

Mfano mmoja suala la chanjo ya ugonjwa wa uviko uliingia katika kipindi kifupi cha mwezi mmoja ulifanya jambo sahihi la kubadilisha uamuzi ambao ulikuwa ni sahihi kubadilishwa. Hilo lilihitaji ujasiri na sio watu wote wangeweza kufanya hivyo.

Hilo peke yake mheshimiwa Rais linatosha kwa sisi kusema unastahili kuendelea kuwa kiongozi wa nchi yetu,” January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 

3. BUSARA YAKO INATAKA UENDELEE KULIONGOZA TAIFA LETU

“Mheshimiwa Rais tunafahamu ulichukua nafasi hii ukiwa Makamu wa Rais. Mimi nilipata bahati ya kuwa Waziri katika ofisi yako ya Makamu wa Rais. Nafahamu jinsi baadhi ya watu pale mjini na ndani ya serikali walivyokuwa wanatuchukulia tulivyokuwa katika ofisi ile.

Hata salamu wengine zilikuwa zinagomba kwa sababu iliaminika hakuna unachoweza kuwapa. Mheshimiwa Rais ulivyochukua nafasi pamoja na kuwajua uliwapa nafasi, uliwaamini kwa sababu nchi iliwahitaji wafanye kazi.

Hilo Mheshimiwa Rais linahitaji busara ya hali ya juu na hekima ya hali ya juu. Na hilo peke yake hata usipochanganya na mengine linatosha kwa sisi uendelee kuwa kiongozi wa nchi yetu,” January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

4. KURUHUSU MIKUTANO YA KISIASA KULIHITAJI MOYO WA ULEZI

“Mheshimiwa Rais uliingia madarakani katika mazingira magumu kidogo ya kisiasa. Kulikuwa na mgawanyiko, tulikuwa tumetoka kwenye uchaguzi uliokuwa umetugawa. Ndio ukweli wenyewe kuna watu waliokuwa wamefungwa, kuna watu walionyang’anywa pesa.

Kuna watu walioharibiwa biashara zao. Mikutano ya hadhara ilizuiwa. Mheshimiwa Rais ukaanzisha maridhiano ya kisiasa ambayo yalipelekea nafasi ya kisiasa kufunguka, watu kufanya mikutano, kusema waliokuwa wanataka kusema.

Biashara zikafunguliwa maisha yakaendelea. Ilihitaji moyo mkubwa wa ulezi wa nchi,” January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

5. RAIS SAMIA AMEREJESHA HESHIMA YA NCHI YETU KIMATAIFA

“Ulichukua uongozi wa nchi wakati hali ya mahusiano ya nchi na Dunia kwa ujumla yakiwa chini kabisa. Watu walikuwa hawaji na sisi hatutoki. Mheshimiwa Rais umerejesha heshima ya nchi yetu.

Muda unaoombwa wewe kwenda duniani ungekuwa unapokea maombi yote ungekuwa hukai ndani ya nchi hata kwa wiki moja. Na wageni wengi wanakuja ndani ya nchi yetu. Umerejesha heshima ya nchi yetu. Hili lilihitaji maarifa ya hali ya juu.

Na hili peke yake linatosha kusema uendelee kuwa kiongozi wan chi yetu,” January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

6. RAIS SAMIA AMEKUZA UWEKEZAJI KUTOKA DOLA BILIONI 1 HADI 5.6

“Ulichukua uongozi wa nchi wakati hali ya uchumi wetu ukiwa umedorora. Uwekezaji ukiwa umeshuka na makusanyo yakiwa chini. Mwaka 2020 mtaji uliokuja kuwekezwa nchini ni Dola Bilioni moja. Mwaka jana 2023 mtaji uliokuja kuwekezwa nchini ni Dola Bilioni 5.6.

Kodi na kazi zimeinufaisha nchi yetu. Makusanyo yaliyoongezeka yamewezesha miradi ifanyike na huduma za jamii zifanyike. Hili lilihitaji akili kubwa na maarifa makubwa.

Mheshimiwa Rais hili peke yake hata usipochanganya na mambo mengine yanatufanya kusema uendelee kuwa kiongozi wa nchi yetu baada ya 2025,” January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

7. UONGOZI WA RAIS SAMIA UMEKWAMUA MIRADI YOTE YA KIMKAKATI

“Mheshimiwa Rais ulipokea miradi ya kimkakati ya gharama kubwa. Reli, Bwawa la Mwalimu Nyerere, mradi wa ndege, mradi wa Busisi, mabarara ambayo yalihitaji fedha nyingi na usimamizi bora zaidi.

Lakini wakati huo huo ulihitajika kupeleka huduma za kijamii afya, elimu bure nk. Uliweza kuyafanya yote. Hakuna mradi uliosimama, mingine inakaribia kukamilika. Umeanzisha mipya, kazi vijijini zinaendelea.

Mheshimiwa Rais hili lilihitaji maarifa makubwa na peke yake inatufanya tuseme uendelee kuwa kiongozi wan chi yetu,” January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

8.AMANI NA UTULIVU WA NCHI NI MATUNDA YA RAIS SAMIA

Mheshimiwa Rais nguzo kuu na sifa ya nchi yetu ni amani, umoja, usalama, utulivu, mshikamano. Bila haya hakuna chochote. Mheshimiwa Rais na sehemu ya kiapo chako ilikuwa ni kudumisha umoja wa nchi yetu katika kipindi ambacho umekuwa kiongozi wetu nchi imekuwa na amani, imekuwa na usalama, imekuwa na utulivu.

Umeamuru majeshi yetu na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kulinda mipaka yetu, kulinda amani yetu. Mheshimiwa Rais kazi hii pia ya Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi umeifanya vizuri na unastahili uendelee kuwa kiongozi wa nchi yetu,” January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

9. UONGOZI WA RAIS SAMIA UMELETA UTULIVU NDANI YA CCM

“Katika sehemu ambayo kuna siasa, hakuna sehemu yenye siasa zaidi ya ndani ya Chama Cha Mapinduzi na hasa ukiwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambacho ndio kiini cha siasa. CCM ni kokoro linabeba watu wa aina zote.

Na kuwaongoza watu hawa katika umoja wao, utulivu wao inahitaji maarifa makubwa sana. Kwa sababu tumo wengi mle ndani. Kila mmoja ana mambo yake. Na kuna maneno mengi kweli kwenye CCM. Mheshimiwa Rais umeyapokea tunayosemana ndani ya CCM.

Ya uongo umeyapuuza, ya kweli umeyafanyia kazi. Ulezi wako wako na uvumilivu wako wa maneno maneno ndani ya CCM umewezesha kuiwe na utulivu ndani ya chama chetu,” January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wadau wafanikisha ujenzi Kituo cha Polisi Mbokomu
44 Wafariki kwa moto uliozuka Ghorofani