Mungano wa asasi za kiraia nchini Senegal (Aar Sunu Election), umetangaza kuundwa kwa umoja mpya na vyama vya kisiasa, ili kutayarisha uchaguzi wa rais kabla ya Aprili 2, 2024.
Kupitia taarifa yake iliyosambazwa kwa vyombo vya Habari, Muungano huo umeeleza kuwa umoja huo mpya utaruhusu kuendeleza hatua na juhudi za pamoja kuzuia juhudi za mapinduzi ya kikatiba yaliyopangwa na serikali.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wagombea 16 kati ya 19 wa upinzani waloidhinishwa na Baraza la Katiba kugombania kiti cha rais katika uchaguzi uloahirishwa Februari 25, wameungana na kuunda umoja unaojulikana kama F24.
Tayari Rais Mack Sall almethibitisha kwa mara nyingine kuwa ataondoka madarakani ifikapo April 2, 2024 na kutangaza kwamba mazungumo ya kitaifa yaliyomalizika yamependekeza uchaguzi wa rais wa nchi utafanyika June 2, ikiwa ni miezi miwili baada ya muda wake kumalizika.