Mataifa zaidi Duniani ikiwemo Uturuki, China, Saudia Arabia, Misri, Jordan yameungana na Umoja wa Mataifa kulaani mauaji ya zaidi ya Wapalestina 100, yaliyofanywa na vikosi vya Israel hapo jana Februari 29, 2024.

Taarifa za vyombo vya Habari, zinaeleza kuwa vikosi vya Israel viliwashambulia kwa risasi kundi la wakazi wa Gaza waliokuwa wakisubiri msaada wa chakula.

 

Hata hivyo, Israel inqsema idadi kubwa ya watu walikufa kutokana na msongamano kwenye eneo la kusubiri chakula na kwamba wanajeshi wake walifyetua risasi baada ya kuona wanatishiwa usalama na kundi hilo.

David de Gea kuibukia FC Barcelona
Eto’o: Song hatasaini mkataba mpya