Beki kisiki wa Liverpool Andy Robertson, ni mmoja wa mastaa wanaowindwa na Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili akazibe nafasi ya Alphonso Davies anayedaiwa kwamba yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na Real Madrid.

Vigogo wa Bayern wanaamini itakuwa kazi ngumu kuipata saini ya Robertson mwenye umri wa miaka 29 mwisho wa msimu huu, lakini wanataka kupambana kuhakikisha wanamsajili.

Beki huyu anatarajiwa kutimiza umri wa miaka 30, mwezi ujao lakini licha ya umri wake bado anaonekana kuwa mmoja kati ya wachezaji bora kwenye kikosi cha Liverpool na Ligi Kuu England, jambo linalowapa matumaini Bayern kuamini anaweza kwenda kuziba pengo la Davies.

Hadi sasa Robertson, amecheza mechi 280 za michuano yote na ameshinda mataji yote makubwa. Kwa sasa beki huyo amebakisha miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2026.

Kafika msimu huu amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara yaliyosababisha acheze mechi 15 za michuano yote.

Mauricio Pochettino: Bado nipo sana
Pawasa: Tunautaka ubingwa COSAFA