Wapinzani wa Chelsea wanafahamu wazi miamba hiyo ya Stamford Bridge itawafungulia mlango wa kutokea mastaa kibao itakapofika Juni 30 mwaka huu, ili kwvenda sawa na ishu ya Financial Fair Play.

Chelsea imetumia zaidi ya Pauni l bilioni kwenye usajili tangu ilipoanza kuwa chini ya mmiliki mpya, bilionea Todd Boehly mwaka 2022.

Usajili wao mkubwa hauendani na wanachovuna ndani ya uwanja, ambapo kikosi hicho kipo mbali sana na Top Four kwenye msako wao wa kutafuta nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao 2024/25.

Ishu ya mapato na matumizi imekuwa siriazi kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ambapo klabu ya Everton imekatwa pointi sita baada ya kuonekana kwamba ilizidisha matumizi.

Ili kukwepwa kukumbwa na kilichowakuta Everton, Chelsea italazimika kuuza wachezaji wake ikiwamo kadhaa waliokuwa wamebeba matumaini makubwa kwenye kikosi cha kwanza.

Na kinachoelezwa ni kwamba Chelsea italazimika kuuza kabla ya kufika Juni 30 mwaka huu, ili kuchangisha Pauni 100 milioni ambayo itawaweka sawa kwenye vitabu vyao vya mapato na matumizi.

Tarehe hiyo iliyotajwa itakuwa katikati ya michuano ya Euro 2024 na Copa America, hivyo Chelsea itakuwa kwenye purushani kubwa kwenye masuala ya usajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Taarifa za kutoka ndani ya Chelsea zinadai kwamba wachezaji wengi watauzwa kwenye dirisha lijalo ili kuleta wachezaji wengine wenye vipaji bora zaidi.

Miongoni mwa mastaa ambao watafunguliwa mlango wa kutokea ni pamoja na Mshambuliaji Romelu Lukaku, ambaye imeelezwa dau la Pauni 37 milioni limeshakubaliwa ili ajiunge jumla AS Roma, licha ya kwamba Chelsea ililipa Pauni 99.5 milioni kunasa saini yake mwaka 2021.

Wachezaji wengine ambao safari inaweza kuwahusu ni lan Maatsen, Reece James, Conor Gallagher, Trevoh Chalobah, Armando Broja, Marc CuCurella na Kepa Avtizabalaga.

Mke wa Pogba afunguka sakata la mumewe
Mama Mbappe anatafuta nyumba Madrid