Gwiji wa soka nchini England Wayne Rooney amefichua kuwa kocha wa Manchester United ni kazi ya ndoto kwake licha ya maisha yake ya ukocha kukumbana na kikwazo baada ya kutimuliwa Birmingham City.
Rooney ndiye mfungaji aliyeweka rekodi ya mabao 253 katika kipindi cha miaka 13 ya uchezaji wake pale Old Trafford.
Kisha alianza hatua inayofuata ya safari yake ya soka kwa kuwa kocha mchezaji pale Derby County, kabla ya kurejea klabu yake ya zamani ya D.C. United na kisha kuwa na siku 83 za kuinoa Birmingham.
Nahodha huyo wa zamani wa England alifikisha umri wa miaka 38 Oktoba mwaka jana na bado ana uwezekano wa miongo kadhaa ya kufundisha na usimamizi mbele yake.
Kwa hiyo, anabakia na matumaini ya kupata kazi nyingine na hatimaye kufanya kazi yake hadi kileleni mwa mchezo kwa wakati ufaao.
“Kwa hakika nataka kurejea kwenye uongozi. Lengo ni kusimamia katika Ligi ya England,
“Manchester United au Everton ndio kazi ya ndoto yangu, lakini ni mchakato,” alisema Rooney akinukuliwa na BBC One.
“Katika miaka kumi ijayo, natumaini naweza kuwa na nafasi ya kuchukua moja ya kazi bora.
“likuwa ni kikwazo kilichotokea Birmingham, lakini mimi ni mpiganaji.
“Unajua kama kocha sehemu ya kazi inafukuzwa na kuwa na vikwazo na ni jinsi unavyorudi nyuma. Labda muda haukuwa sawa nilipoingia nikiwa Birmingham, mashabiki hawakunikubali kuanzia siku ya kwanza.”