Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania ‘CHANETA’ Bi Rose Mkisi amejiuzulu nafasi yake baada ya sakata la kuishutumu Serikali kwa upendeleo.
Mkisi alinukuliwa na Redio moja akisema Serikali inapendelea sana mpira wa miguu na kwamba wameisahau michezo mingine ikiwemo Netiboli.
Mkisi mbali na kusema kwamba soka walipewa pesa kwenda kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ jambo ambalo Waziri wa Sanaaa Utamaduni na Michezo alilipinga vikali na kutoa amri kwa Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa Bi Neema Msita kuhakikisha anamfikisha Rose Mkisi kwenye Kamati ya nidhamu akajieleze kuhusiana na tuhuma zake kwa Serikali.
Waziri Ndumbaro alitoa maagizo hayo kwenye hafla ya kuziaga timu zinazokwenda ALL AFRICANS GAMES iliyofanyika kwenye moja ya kumbi za uwanja wa Benjamin Mkapa.
Waziri Ndumbaro alikataa hata kujumuika na viongozi wa CHANETA kwenye kikao cha viongozi wa vyama vya michezo na yeye kilichokuwa kifanyike jana Jumanne (Machi 05).
Katika barua yake ya kuthibitisha kujiuzulu Rose Mkisi ameandika: Nimeamua kujiuzuru nafasi ya Katibu Mkuu CHANETA kutokana na sintofahamu kuhusu maandalizi ya timu ya mpira ya pete inayojtandaa kushirtki mashindano ya U 21 yanayotarajia kufanyika Afrika ya Kusini.
Nimefikia uamuzi huu kwa maslahi mapana ya Taifa na maendeleo ya mpira wa pete nchini.