“Nawatakia kheri ya maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani.” Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri.

Kihistoria, kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, kimekuwa kikiadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8 huku jamii ikitambua mafanikio ya Wanawake bila kujali Utaifa, ukabila, udini, utamaduni, lugha, hali ya kiuchumi au mwelekeo wa kisiasa.

Rasmi siku hii iliasisiwa mwaka 1908, wakati wanawake 15,000 walipoandamana katika jiji la New York Nchini Marekani wakidai muda mfupi wa kazi, mishahara bora na haki ya kupiga kura.

Kwa mwaka huu (2024), siku ya Wanawake inaenda na kauli mbiu isemayo “Wekeza kwa Mwanamke, kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa Jamii.”

Hapa Nchini tunayo Sekta ya Maji iliyo chini ya Wizara ya Maji. Hapo kuna ujumbe maalum ambao umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, akisema anawatakia kheri ya maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani.

 

Dkt. Mfaume atoa mwezi mmoja Hospitali ya Mlele
TEEMO waadhimisha siku ya Wanawake kwa uzinduzi