Baada ya sekeseke lililochukua nafasi kuhusu kitita kipya cha bima ya afya kilichotangazwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kupingwa na Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA) sasa kikao cha maridhiano kuanza jumatatu ijayo kutatua sakata hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga amesema jumatatu wataingia kwenye majadiliano rasmi kutafuta muafaka kwa yale maeneo ambayo yana changamoto.

Amesema, “tuna miaka nane hatujafanya mapitio yamfuko wa bima ya afya kwenye kitita cha mafao, kupitia mapitio hayo tumekuta kuna dawa mwaka 2016 ilikuwa inauzwa milioni nne sasa imeshuka hadi laki tisa, je tukiendelea kulipa milioni nne laki mbili, tutakuwa hatutendei haki hela za wanachama.”


Mgogoro wa juzi ni baada ya sisi kufanya mapitio kwa kushiirikiana nao, tulipotaka kutangaza sasa wanaweza wakatoa maoni yao tena kwa Waziri Mwenye dhamana, maana yeye ndiye anatoa idhini kabla ya kutoa idhini akaunda kamati ya wataalamu, kamati ikafanya kazi yake , ikaja na vigezo vyake ikaja na vigezo muhimu ikafanya mapitio na kuweka sawa kipi cha kutekelezwa ila wao bado wakawa na sababu zao.” Amesema Konga na kuongeza kuwa.

“Baada ya hapo nashukuru wao walikaa chini kutokana na kauli ya Mhe Waziri kuwasihi waendelee kutoa huduma, warudi mezani, baaada ya siku mbili walitangaza kurejesha huduma natukakaa nao vikao huduma inaendelea na majadiliano yananza rasmi siku ya jumatatu na tunaamini tutapata muafaka kwa yale maeneo ambayo yana changamoto yatarekebishwa na maeneo yatayohitaji ufafanuzi utatolewa,” amesema Konga.

Katika hatua nyingine amezungumzia changamoto ya kutofautiana picha kwenye kadi za NHIF na usumbufu unaojitokeza kwa wananchi Mkurugenzi wa NHIF amekiri wazi kuwa ni kweli.

“Tuko wakali sana kwenye hilo zoezi, tulichokuja kugudua kuna wimbi kubwa la watu kupokezana kadi, tunafanya kazi yetu. Huwezi kumlaumu leo Trafiki kwanini anasimamisha magari anakagua, taili si kipara usije kupata ajali mbele, sasa sisi tunakuta watu wanaiba, mtu anachukua kadi ya mtoto huyu anaenda kumtibia mwingine, hizi elfu 54 wanazolalamikia unakuta inatibu watoto wanne ndani ya familia.”

Alisema, Ukienda kwa mtoa huduma yeye hana sababu ya kukagua kadi yeye anachoangalia hela inaingia, ndio maana tumeweka watu wetu kwenye hivyo vituo na hatutarudi nyuma, tumeweka kwa muda ila tunakuja na mfumo ambao utakua unakagua kwa vidole, ukienda sura inagoma ule ni udhibiti kuwa hela ya wananchama inaenda kwa wanaostahili.”

“Tutaendelea kuwa wakali vinginevyo hiyo asilimia 8 tutatibu asilimia 15, tuko wakali tunasimamia karibia vituo vyetu vyote tumeweka watu. Kama mtoto wako amekuwa nenda kabadilishe picha yake weka ya sasa. Lakini tukigundua mtoto na kadi haviendani tutakamata kama mharifu na kuchukuliwa hatua nyingine, vinginevyo huu mfuko utaibiwa, lazima tujirishidhe,” amesema Bernard Konga.

Aweso awatumia salaam za heri Wanawake
Dkt. Mfaume atoa mwezi mmoja Hospitali ya Mlele