Waziri wa Maji Jumaa Aweso leo Machi 8 2024, amewatakia kheri ya siku ya Wanawake wote nchini.
Siku hii ya Kimataifa ya Wanawake, ni kampeni ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa ya kuhamasisha juhudi za kuleta usawa wa kijinsia duniani kote.
Kwa mara ya kwanza, iliadhimishwa mwaka 1911, katika nchi za Austria, Denmark, Ujerumani na Uswizi.
Umoja wa Mataifa – UN, ulianza kuadhimisha siku hii mwaka 1975 huku kaulimbiu ya kwanza iliyopitishwa na UN (mwaka 1996), ikiwa ni “Kuadhimisha yaliyopita, Kupanga kwa ajili ya baadaye”.