Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia Mkuu wa kituo cha Police Loliondo, ASP Fatma Juma katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani ametoa elimu kwa makundi ya Akina mama na wanaume juu ya madhara ya ukatili wa Kijinsia kwa jamii wa Kifugaji.

Katika elimu hiyo, Polisi imewaonya baadhi ya Wananchi wa jamii ya kifugaji ambao wanajihusisha na vitendo vya ukatili kwa Wanawake na Watoto kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

ASP Fatma, ameeleza kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwepo la Pastrol Wowens Council (PWC), yameendelea kushirikiana na Serikali katika kupinga ukatili dhidi ya mama na mtoto ambayo yameshamiri sana katika jamii na kuwaomba waendelee kutoa elimu ili kusaidia jamii.

Dawati la Jinsia la Polisi Tanzania, limekuwa likiendelea na juhudi zake za kuhakikisha linatoa elimu kwa jamii juu ya masuala mbalimbali ya ukatili kwa Wanawake na Watoto nchi nzima, sambamba na ile ya ulinzi wa raia na mali zao.

Wafugaji kuondokana na tatizo la uhaba wa malisho
Rais Samia: Nchi ikiwa na amani Mungu anashusha baraka