Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema dhamira ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wafugaji wanafuga kisasa na ndio maana amewapelekea mbegu za malisho, ili wafugaji waondokane na changamoto ya malisho hapa nchini.

Waziri Ulega ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi mbegu za malisho kwa wafugaji wa kijiji cha Msomera wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya sekta ya mifugo katika kijiji hicho kilichopo wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Amesema, “kwa hivyo kazi kwenu wafugaji, amekupeni mbegu hizi zenye thamani kubwa ili muweze kupanda na nikija hapa tena baada ya mvua nikute mashamba ya malisho yameenea,” alisema.

Aidha, Ulega amewataka wafugaji hao watakapo panda na kuvuna malisho yao kuhakikisha wanaweka akiba ili yaweze kuwafaa wakati wa kiangazi huku Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania, (CWT), Murida Mushota akiwataka Wafugaji kutumia mbegu hizo kuleta mabadiliko kwenye sekta ya mifugo.

Ifahamu mbinu ya kudhibiti ushirikina katika biashara yako
Ukatili: Jamii ya Kimasai yaonywa