Mahakama ya jijini Kigali imemuhukumu raia wake Denis Kazungu, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya watu kadhaa, ambao miili yao ilikutwa imezikwa nyumbani kwake.

Kazungu alikamatwa Septemba 2023, baada ya Polisi kufanya msako nyumbani kwake jijini Kigali na kugundua miili ya watu hao.

Kuhukumiwa kwake kunafustia ushahidi ulikutwa nyumbani kwake na pia alikiri kuwauwa Wanawake 13 na Mwanaume mmoja, akidai walimuambukizwa virusi vya Ukimwi.

Aidha, Kazungu alipokamatwa, alisema aliwarubuni watu hao na kwenda nao nyumbani kwake, kisha kuwabaka, kuwaibia na kuwaua.

Septemba 21, 2023, Kazungu alikiri makosa ya mauaji hayo na alihukumiwa kifungo cha maisha jela Machi 8, 2024.

Ujenzi Miradi ya Maendeleo: SMZ yapongeza Vikosi
Wajipanga kuleta mapinduzi sekta ya Elimu