Baraza kuu la usalama katika Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Sudan katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadan.
Baraza hilo, limesema hatua hiyo ya kusitishwa kwa vita pia itasaidia raia milioni 25 wanaohitaji chakula kuweza kufikiwa na msaada.
Mamia ya raia wa Sudan wamekimbilia katika nchi jirani ikiwemo Chad, kwa hofu ya kushambuliwa katika mapigano yanayoendelea kati ya pande mbili za kijeshi.