Chama tawala Nchini Rwanda, Rwandan Patriotic Front (RPF), kimemteua Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame kuwa mgombea wa uchaguzi wa urais unaotarajia kufanyika Julai 15, 2024 kwa muhula wa nne wa miaka saba.
Kwa mujibu wa uamuzi wa mwaka jana (2023), wa Serikali, Rwanda inapanga kufanya uchaguzi wake huo wa urais na wa wabunge katika tarehe hiyo na uamuzi wa Mahakama uliopangwa kufanyika Machi 13, 2024 ndio utakaoamua iwapo Kagame ameidhinishwa kuwania urais.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda imesema Wabunge Wanawake 23, Wawakilishi wawili wa Vijana na Mwakilishi mmoja wa Watu wenye ulemavu pia watachaguliwa na vyuo na kamati za uchaguzi hapo Julai 16, ambapo Wagombea watafanya kampeni kuanzia Juni 22 hadi Julai 12, 2024.
Kamage (66), ameitawala Rwanda kwa mkono wa chuma tangu katikati ya miaka ya 1990 na kushinda uchaguzi wa urais, kila mara kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura, katika chaguzi za mwaka 2003, 2010 na 2017.