Inaelezwa kuwa Klabu ya Brentford itatakiwa kushusha bei ya Mshambuliaji wao, Ivan Toney dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuvutia timu mbalimbali zinazohitaji saini ya nyota huyo.

Brentford italazimika kumuuza nyota huyo wa kimataifa wa England kwa bei ya chini na msimu huu akiwa amecheza mechi tisa tu kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na kesi iliyokuwa ikimwandama pamoja na kufungiwa kujihusisha na soka.

Toney ambaye mkataba wake unamalizika mwakani, anawaniwa na miamba ya soka England ikiwamo Arsenal na Chelsea na endapo Brentford itazembea kumuuza dirisha lijalo la majira ya kiangazi huenda ikamuuza kwa hasara dirisha la majira ya baridi mwakani.

Awali ilidaiwa Brentford ilikuwa ikihitaji zaidi ya Pauni 70 milioni, lakini ifikapo mwisho wa msimu inaonekana kuwa ngumu kumuuza Toney kwa kiasi hicho cha pesa kwa sababu mkataba wake utakuwa unakaribia ukingoni.

Toney amerejea kwenye kikosi cha Brentford mwaka huu baada ya kufungiwa kwa miezi nane kujihusisha na soka kwa kosa la kujihusisha na masuala ya kamari ‘Kubeti’, huku Chelsea na Arsenal zikipambana kuiwania saini yake ili akaongeze ubora kwenye safu zao za ushambuliaji.

Mawaziri SADC watuma salamu za rambirambi JMT
Matola: Msitutoe kwenye mbio za ubingwa