Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amewasili rasmi ofisini na kuahidi kumsaidia Rais, Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa.
Mara baada ya kuwasili Ofisi za Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma, alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mha. Felchesmi Mramba, menejimenti na watumishi wengine wa Wizara ya Nishati.
Akizungumza baada ya mapokezi hayo, Dkt. Mataragio amesema ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi ni nyenzo muhimu ya kuyafikia matarajio ya viongozi wa kitaifa na Taifa kwa ujumla.
Amesema, “mimi nashukuru kuteuliwa kutumikia nafasi hii, nitaendelea kushirikiana na watumishi wenzangu ili kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake.”
Zifuatazo ni baadhi ya Picha za kumbukumbu wakati Dkt. Mataragio alipowasili ofisini hapo.