Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umekamilisha tathmini ya awali ya vihatarishi vya usalama na afya katika eneo la mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Mwl. Julius Nyerere (JNHP), lililopo Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema kwa mujibu wa kifungu Na. 60 cha Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003, wamiliki/wasimamizi wa sehemu za kazi wanawajibika kuhakikisha kwamba maeneo yao ya kazi yanafanyiwa tathmini ya vihatarishi vya usalama na afya walau mara moja kwa mwaka, ili kupata taarifa muhimu zinazohitajika katika kuandaa mikakati madhubuti ya kulinda uwekezaji na kuwakinga wafanyakazi dhidi ya athari za vihatarishi katika eneo la kazi husika.

Amesema, “ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa matakwa ya sheria tajwa, mwaka 2022, Shirika la Umeme (Tanesco) kwakuzingatia uzoefu wetu na uwepo wa wataalam wa kutosha waliobobea katika masuala ya usalama na afya kazini, lilituomba kufanya tathmini ya awali ya vihatarishi katika eneo la mradi na kutoa ushauri elekezi wa uimarishaji wa mifumo ya kudhibiti vihatarishi mahali pa kazi.”

“Hivyo, baada ya wataalam wangu kukamilisha kazi niliyowatuma nami nimeona ni muhimu kufika katika eneo la mradi kuona kama kazi hiyo imefanyika kikamilifu”. Amesema Mwenda.

Mwenda ameongeza kuwa, “hatua iliyochukuliwa na serikali yetu kutekeleza mradi huu wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji (hydropower generation) ni ya msingi sana na yenye tija kubwa katika kuchagiza ukuaji wa uchumi hapa nchini.”

Vurugu zamuondoa Waziri Mkuu madarakani
Sitisho la mapigano mwezi Mtukufu lakwama