FC Barcelona imekataa ofa euro milioni 200, iliyotumwa na Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain iliyoonesha nia ya kumsajili kiungo Mshambuliaji Lamine Yamal Nasraoui Ebana.

PSG wanajiandaa kumsajili kiungo huyo kutoka Hispania ili kuziba pengo la Kylian Mbappe, ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya kumalizika kwa mkataba wake na anatarajiwa kujiunga na Real Madrid.

Licha ya kumpoteza Mfaransa huyo kwa uhamisho wa bure, makubaliano ya kisheria kati ya klabu na mchezaji huyo yatamfanya Mbappe kulipa hadi euro milioni 80 atakapoondoka.

Kuondoka kwa Mbappe pia kutaifanya PSG kuokoa karibu euro milioni 200 kila mwaka, na kuwaacha na fedha nyingi kusajili mbadala wa jina kubwa.

Na kwa mujibu wa gazeti la Marca, PSG wameweka macho yao kwa Yamal mwenye umri wa miaka 16, ambaye ameibuka kama mchezaji muhimnu wa Barcelona msimu huu, akifunga bao lake la sita msimu huu, ljumaa wakati Barca wakiibamiza Mallorca kwenye La Liga, ambapo alijikuta akifananishwa na Lionel Messi.

Aina hiyo ya vipaji, ndivyo PSG wanatafuta na inasemekana waliweka wazi kwa Barcelona kwamba watakuwa tayari kulipa euro milioni 200 ili kumnasa Yamal kwenda Ufaransa wakati wa usajili wa msimu wa majira ya joto.

Wakala wa Yamal, Jorge Mendes, alikutana na rais wa Barcelona, Joan Laporta, mapema juma hili kujadili mada kadhaa na pendekezo hili kutoka kwa PSG kwenye ajenda.

Barcelona, ambao tayari walikuwa na ufahamu wa kutoka kwa PSG, waliweka wazi kwamba hawana mpango wa kumuuza Yamal msimu huu wa majira ya joto.

Wakiwa na wasiwasi wa aina ile ile ya uwezo wa kifedha ambayo PSG ilianzisha kifungu cha Neymar cha euro milioni 222 mnamo 2017, Barcelona iliingiza kifungu cha kumnunua cha euro bilioni moja katika mkataba wa miaka mitatu aliosaini Lamal mwaka jana.

Kuhusu PSG kutafuta mbadala wa Mbappe, imefahamika kuwa Marcus Rashford wa Manchester United na Victor Osimhen wa SSC Napoli pia ni wachezaji wanaozingatiwa.

Kimmich: Sina papara na mkataba mpya
Vitita vya Mafao: NHIF, APHFTA warudi mezani