Vyombo vya Moto, (Pikipiki 23 na Magari 11)  vimekabidhiwa kwa Taasisi na Wizara zinazotekeleza Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi Nchini.

Hafla hiyo imefanyika hii leo Machi 12, 2024 Jijini Dodoma, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Muhagama amesema vitendea kazi hivyo vimegawiwa kwa Wizara ya  Kilimo Gari moja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Magari manne.

Vingine ni Pikipiki 16 ambapo tatu za miguu mitatu, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo -TARI Magari mawili na pikipiki 4 na Wakala wa Mbegu za Kilimo ASA Magari matatu na pikipiki 3 za miguu mitatu.

Amesema, malengo ya Programu ni kufikia kaya zenye kipato cha chini zipatazo laki mbili na sitini (260,000) kwa lengo la kuwaongezea kipato, lishe bora na usalama wa chakula na shughuli hizi mbalimbali zinatekelezwa  na Wizara, Taasisi mbalimbali na halmshauri.

“Na shughuli hizi ni pamoja na utafiti, uzalishaji na usambazaji wa mbegu za mazao ya Kilimo hususan Alizeti, Mahindi, Maharage na mimea jamii ya kunde ikijumuisha na mafunzo ya matumizi bora ya mbegu na mazao hayo”, amesema Mhagama.

Shughuli nyingine ni utafiti na uzalishaji wa vifaranga vya samaki, uvuvi wa bahari kuu, mafunzo ya ufagaji wa viumbe maji, uongezaji thamani mazao ya samaki na uzalishaji wa mwani huku akisema Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kusimamia na kuratibu Programu hiyo kwa umahiri ili malengo yaliyokusudiwa yafikiwe kwa wakati.

Tajiri Man Utd kuanza na huyu
Kimmich: Sina papara na mkataba mpya