Johansen Buberwa – Kagera.

Shirikisho la Soka Nchini – TFF, limegawa mipira 700 kwa katika shule za Msingi za Wilaya Saba ndani ya Mkoa wa Kagera, kikilenga kukuza vipaji vya soka.

Akizungumza wakati wa kugawa vifaa hivyo, Afisa Michezo na Utamaduni Mkoani humo, Khefa Elias amesema ndani ya Mkoa huo umeanza kutambua umuhumu wa sekta ya michezo ambapo Wilaya za Kyerwa, Karagwe na Missenyi zimeanza kujenga Viwanja vya michezo.

Amesema Mkoa huo bado una changamoto ya Bajeti, Walimu wachache wa Michezo, uhaba wa Vifaa vya Michezo kwenye Shule na tatizo la Viwanja vya michezo kuvamiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Cha cha Soka Mkoa wa Kagera – KRFA, Salum Chama amesema nia ya kugawa mipira hiyo, ni kuongeza chachu ya kukuza kiwango cha soka na kuibua vipaji vya watoto wa shule kuanzia umri wa miaka 15 hadi 20 na kila wilaya itapata mipira 100.

Awali, Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajath Fatma Mwassa amesema wadau wa michezo na Viongozi wanapaswa kuunga mkono juHudi za TFF kwa kushirikiana na KRFA na kuwataka wasimamizi wa michezo watumie mipira hiyo kuwa chachu ya michezo.

Aidha, Sima aliwataka Wakurugenzi wa Halmashari zote za Mkoa wa Kagera kutenga fedha kwa ajiri idara ya michezo, Walimu na kupewa mafunzo yatakayo weza kuongeza ufanisi katika michezo kwa kukuza vipaji.

Dereva ulisifuate Basi kwa nyumba linapo 'overtake'
23 kizimbani kwa kujihusisha na biashara ya Dawa za kulevya