Klabu ya Chelsea inajiandaa kushirikiana na Saudi Arabia katika kipindi cha majira ya joto baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo, Todd Boehly kukutana na Michael Enmenalo wakati wa ziara yake ya hivi karibuni.
Emenalo ni mkurugenzi wa soka wa Ligi Kuu ya Saudia, ambaye huko nyuma alikuwa akishikilia nafasi hiyo katika klabu ya Chelsea.
Mkutano huo ambao ulifanyika Riyadh majuma mawili yaliyopita, umeibua tetesi Chelsea kutaka kuwaachia baadhi ya wachezaji wake kwenda Saudia kucheza soka.
Pia inaelezwa kuwa Riyadh Air imekuwa ikihusishwa na kuja kuwa mdhamini mpya wa jezi wa klabu hiyo msimu ujao.
Chelsea iliwapiga bei Kalidou Koulibaly na Edouard Mendy kwa klabu ya Al-Hilal na Al-Ahli katika kipindi kilichopita cha majira ya joto, ili kuchangisha kiasi cha ada ya Pauni milioni 33 (sawa na Sh bilioni 107), wakati N’Golo Kante alijiunga na Al-Ittihad bure.
Chelsea katika kipindi hiki cha majira ya joto inaangalia kuwaacha nyota wake kama Romelu Lukaku, Kepa Arrizabalaga, Armando Broja, Trevoh Chalobah, Marc Cucurella na Raheem Sterling.