Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Mwina Kaduguda amesema kuna haja kwa Mashabiki, Wanachama, Viongozi na Wachezaji kushirikiana kwa pamoja, endapo wanahitaji kuifunga Al Ahly katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba SC imepangwa kukutana na Al Ahly katika mchezo wa Robo Fainali utakaopigwa Ijumaa (Machi 29), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kabla ya mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa jijini Cairo-Misri kati ya April 05 na 06.

Kaduguda ambaye kwa sasa yupo nje ya uongozi wa Simba SC amesema kihistoria Al Ahly hajawahi kuifunga klabu hiyo ya Msimbazi, na hiyo imetokana na umoja wa wanasimba hasa unapokaribia mchezo dhidi ya miamba hiyo ya Misri.

“Tangu 1985 Al Ahly akija hapa lazima afungwe na Simba SC atake asitake atafungwa lazima tukubali, Watanzania wengi ambao ni vijana hawaulizi Historia iko na mambo matatu yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Mtu mwenye upeo mdogo anajua Historia ni mambo yaliyopita”

“Barbra amewahi kunitumia ujumbe kuwa Al Ahly wamesema kuwa mwaka huu wanakuja kivingine nikamuambia waambie watafungwa ile mechi tukawafunga 1-0 bao la Miquissone na wakaondoka kwa hasira”

“Kama uongozi utashirikisha watu wengine Al Ahly hatoki hapa Dar es salaam” amesema Kaduguda

Katika hatua nyingine Kaduguda amesema msimu huu Simba SC imefuzu kwenda Robo Fainali kwa kubebwa na kanuni za Michuano hiyo CAF, tofauti na ilivyokuwa ikifanya miaka mitano iliyopita.

Amesema hatua hiyo huenda imetokana na ushindani uliokuwepo katika Kundi B ambalo lilikuwa na timu za ASEC Mimosas (Ivory Coast), Wydad Casablanca (Morocco) na Jwaneng Galaxy (Botswana)

“Mpira lazima ujue unaongea na Nani? Jambo lolote muhimu kujua ambaye unazungumza naye..weledi wake, utaalam wake kwenye fani husika”

“Naheshimu mawazo ya kila mtu, Simba SC msimu huu kwenye makundi tumeingia Kwa kanuni lakini Miaka ya nyuma tulikuwa tukiingia kwa kushinda nje ndani, Lakini mwaka huu tumeingiaje? Kikanuni” amesema Kaduguda

 

CAF kuikutanisha Serikali, TFF, Simba SC, Young Africans
Job afichua ugumu wa kazi yake