Mchezaji wa Kimataifa wa Burundi anayekipiga ndani ya Simba SC, Saidi Ntibazonkiza hataonekana katika mechi mbili za kirafiki ambazo timu ya Taifa ya Burundi Intamba Murugamba wanakwenda kucheza nchini Madagascar Machi 22 na 25,2024.
Imeelezwa kuwa ameomba kutoshiriki mechi hizo za kirafiki kwasabababu zake binafsi.
Katika mechi mbili hizo za kujiandaa na mashindano ya CHAN, kutafuta kufuzu kombe la Dunia 2026 na CECAFA Senior Challenge Cup Meneja wa Intamba Murugamba, Achel Niyongere amefahamisha kuwa mbali ya Saido Ntibazonkiza mchezaji mwingine ambaye hataonekana ni pamoja na Marco Weymas.
Beki kisiki Fredrick Nsabiyumva na Yousouf Nyange anayekipiga Nice ya Ufaransa ni miongoni pia mwa wachezaji ambao hawataweza kujumuika na wenzake nchini Madagascar.
Kikosi cha Timu ya Taifa Intamba Murugamba kinatarajiwa kutangazwa kesho Jumamosi (Machi 16) kabla ya kukwea pia siku ya Jumatatu (Machi 18).