Mwenyekiti wa Jumiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa, Fadhil Maganya ameitaka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknoloknolojia kuacha taibia ya urasimu wa ujenzi wa Vyuo vya VETA Nchini, kutokana na mfumo uliowekwa kuangalia sehemu moja jambo ambalo linasababisha miradi kushindwa kukamilika kwa wakati.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Kata ya Kyerwa Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera, ikiwemo ujenzi wa Chuo cha Ufundi stadi – VETA, Maganya amesema nia ya Serikali ni kujega vyuo hivyo 63 nchini na kusema jitihada zinataka kuingia dosari kutokana na baadhi ya maeneo miradi hiyo kukwama.
Kwa upande wake Mthibiti Ubora Wilaya ya Kyerwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Daniel Balabola amesema eneo hilo lina ukubwa wa hekaRi 14 na gharama ya mradi huo ni bilioni3.5 ambapo bilioni 1.4 itajenga majengo kwa kipindi cha awamu ya kwanza katika majengo tisa.
Amesema, awamu ya kwanza itahusisha jengo la Mlinzi, Utawala, jengo la kuzalishia umeme, Madarasa, Tehama, Karakana tatu, Choo cha nje pamoja na Nyumba ya Mkuu wa chuo, na kwamba mpaka sasa wamepokea shilingi milioni 324 ambayo itakamilisha maboma hayo na kupelekea mradi huo kufikia asilimia 40.