Lydia Mollel – Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amefanikiwa kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya Mwanajeshi mstaafu aliyejulikana kwa jina la Joseph Michael maarufu kama Ndemeka, dhidi ya Wanakijiji wa Mbegesera uliodumu kwa muda mrefu.
Shaka amesema, hatakubali kuona Migogoro ya Ardhi inachukua nafasi katika Wilaya hiyo na kwamba ndani ya miaka mitatu iliyopita hakuna kifo cha mgogoro wa Wakulima na Wafugaji kilichotokea na sasa Migogoro ya Ardhi imeanza kujitokeza jambo ambalo hataruhusu.
Amesema, hakuna mtu aliye juu ya sheria hivyo Wananchi wanatakiwa kuwa na Imani na viongozi hivyo amewataka kuwasilisha changamoto zao bila Kuhofia vitisho wanavyopewa kwakua Asilimia 88 ya mapato wilayani huko yanatokana na Kilimo.
Kufuatia kumalizika kwa mgogoro huo, mkazi mmoja wa Kijiji hicho alifanya maombi maalumu ya kumuombea DC shaka kwa Mwenyezi Mungu, ili aweze kupambana na Wananchi wakorofi wanaosababisha migogoro ya ardhi katika Wilaya hiyo.