Mazingira ya ukosefu wa huduma muhimu za kijamii kama Maji na nyinginezo ambayo ni chanzo cha uharibufu wa mazingira katika baadhi ya maeneo hasa Vijijini, yamepelekea Serikali kuanzisha mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi, kwa kutumia mifumo ya Ikolojia Vijijini EBARR, unaotekelezwa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Shida ya Maji iliyodumu kwa muda mrefu katika Kijiji cha Chagongwe Wilayani humo, ilisababisha wenyeji kukipa Kijiji jipya la KAZANIA na kusema ili kuyapata maji iliwalazimu kukaza nia kwa kuyafuata umbali wa zaidi ya km 10 wakitumia zaidi ya masaa matatu.
Kuna msemo wa waswahili usemao “Hakuna marefu yasiyo na ncha” na sasa msemo huo umejidhihirisha kwa wakazi wa KAZANIA kuishukuru Serikali kwa kuwanufaisha kupitia mradi huo, utakaoendelea kurahisisha maisha, baada ya kuteseka kwa muda mrefu.
Ofisi ya Makamu wa rais, Muungano na Mazingira, inaongozwa na Dkt. Seleman Jafo. Mbali na kwamba alihusika kuzindua Visima vya Maji lakini ilifanya jambo la ziada kuinua uchumi kwa Wananchi, ili wajipatie kipato nje ya shughuli zao za kila siku kwa kugawa Vyerehani 21 kwa vikundi vitatu na kuzindua Joshi za kunyweshea Maji Mifugo.
Mradi wa ABARR, unatarajiwa kunufaisha zaidi ya kaya 29,000 na unakadiriwa kuwafikia wanufaika zaidi ya milioni moja (1,000,000) kupitia utekelezaji wa shughuli za miradi mbalimbali kama vile upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kilimo na ufugaji, shughuli mbadala za kujiongezea kipato; na urejeshaji wa vyanzo vya maji uliogharimu zaidi ya Shilingi bilioni 1.6.
Baadhi ya miradi iliyojengwa kupitia Mradi wa EBARR ni pamoja na Birika za kunyweshea mifugo, Vitalu nyumba, Manzuki (nyumba za nyuki), ununuzi wa Ng’ombe (aina ya Borani), Mbuzi (aina ya Isiolo), Vifaranga vya Kuku, Boti za kisasa za uvuvi zilizonunuliwa Kaskazini A, Visima vya maji pamoja na Shamba Darasa (kwa mazao na ufugaji, uzalishaji wa mbuzi na ng’ombe yameanzishwa, Majosho yaliyojengwa.