Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Dotto Biteko amemtaka Waziri wa Maji kuhakikisha maeneo yaliyotengwa Kwa ajili ya Vyanzo vya maji yanalindwa ili kuondoa hofu ya kuvamiwa kwa vyanzo hivyo vya maji.
Dkt Biteko ametoa agizo hilo Jijini Dodoma katika Maadhimisho ya kilele cha siku ya maji Duniani ambapo ameongeza kwa kusema zipo baadhi ya Taasisi, Mashirika na Wananchi wanaovamia maeneo hayo ya vyanzo maji.
Amesemausalama wa Nchi unategemea maji kama kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya maji mwaka inavyofananua, “Uhakika wa maji kwa amani na utulivu.”
Hata hivyo, ametoa agizo la kuendelea kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi ili kupunguza mzigo wa lawama unaotupiwa serikali.
Aidha, ametoa wito taasisi, mashirika na wananchi kuweka miundombinu ya kuvuna maji katika eneo lake ili kupunguza kero ya upatikanaji wa huduma ya maji.
Mbali na maelekezo hayo, Dkt. Biteko ameshuhudia zoezi la utiaji saini Randama za Mashirikiano (MoU) pamoja na mikataba ya uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira katika mji wa serikali Mtumba.