Afisa Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi Philon Kyetema amethibitisha kuwashikilia Wahamiaji Haramu 20 kutoka nchini Ethiopia, ambao walikamatwa katika kizuizi cha Minjingu Wilayani Babati Mkoani Manyara, wakisafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa kutumia gari binafsi aina ya Toyota Land Cruiser, lenye nambari za usajili T774 BDL.

Kamishna Msaidizi Kyetema ameyasema hayo hii leo Machi 25, 2024 na kudai kuwa tukio hilo lilitokea mACHI 23, 2024 na kudai kuwa wanamshikilia Dereva Edward Erihad mkazi wa Dodoma, kwa tuhuma za kuwabeba wahamiaji hao, ambaye alitumia Bendera ya Chama cha Mapinduzi – CCM kwa kuiweka kwenye gari kama njia mojawapo ya kufanikisha uhalifu huo.

Aidha, ameongeza kuwa, kwasasa bado wanaendelea na upelelezi kuhusu tukio hilo na utakapokamilika watafikishwa Mahakamani, huku chama cha mapinduzi – CCM, Mkoa wa Manyara wakilaani tabia ya wahalifu kutumia jina la chama.

Ronald Araujo: Bado nipo sana
Simba SC yamvuruga kocha Azam FC