Wakati vuguvugu la Shakahola la mafundisho ya kidini ya kupotosha na kupelekea vifo vya zaidi ya watu 220 likiendelea kushika hatamu, wakazi wa kijiji cha Majengo, Kanagoni Kaunti ya Kilifi wanaishi kwa hofu, baada ya kupewa vitisho vya kuhama la sivyo watachinjwa.

Hatua hiyo, inafuatia takriban wakazi 260 kutoka kijiji hicho kulala nje baada ya makazi yao kubomolewa na Bwanyenye mmoja anayedai kumiliki ardhi wanayoishi, huku mzee wa kijiji, Kalume Kazungu akisema ubomoaji huo ulifanyika chini ya ulinzi wa maafisa wa Polisi bila ya wao kupewa ilani ya kuhama eneo hilo.

Amesema, “tumelala nje tukipigwa na baridi. Watoto hawawezi kuenda shule kwa sababu nguo zote zilichomwa na wanaonyemelea hii ardhi yetu wakidai ni yao. Sisi maisha yetu yote tumeishi hapa hadi tuko na watoto na wajukuu lakini leo hii tunakuja kuambiwa tuondoke eti hapa sio kwetu.”

“Tafadhali viongozi wetu, tunaomba utuangalie tuweze kupata haki maana tunaumia. wamekuja na polisi wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa ADU na mkubwa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai Marereni na kubomoa na kuteketeza baadhi ya nyumba sasa tunalala nje,” alisema Kazungu.

Aidha, Kazungu anasema wanapitia changamoto nyingi tangu ubomoaji huo ufanyike na kuongeza kuwa “tuko watu zaidi ya 260 huyu bwanyenye anaitwa Salat, tu familia, mifugo na mashamba tukifanya maendeleo hapa. iweje mtu aje atutatize na kutufurusha akisema ni kwake? nina miaka 70 unifukuze kwangu unataka niende wapi?” aliuliza.

KMC FC yatamba kuisasambua Mbeya City
Naibu Waziri atembelea kituo cha michezo Tanga