Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG, Charles Kichere amewasilisha ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma ambapo na kuzungumzia deni la Taifa ambalo limefikia trilioni 82.25.
CAG Kichere amesema, deni hilo la Serikali ni sawa na ongezeko la asilimia 15 kutoka Trilioni 71.31 kwa mwaka 2021/2022, likijumuisha deni la ndani Trilioni 28.92 na deni la nje Trilioni 53.32 na kusema kipimo kinaonesha deni hilo ni himilivu.
Amesema, “uwiano wa kulipa madeni na mauzo ya nje ni asilimia 12.7 chini kidogo ya kiwango cha ukomo cha asilimia 15 na uwiano wa malipo ya madeni na mapato ni asilimia 14.3 chini kidogo ya kiwango cha ukomo elekezi cha asilimia 18.
Aidha, akatika ripoti hiyo iligundulika pia Mashirika nane ya umma yalikusanya mapato ya Shilingi Bil. 23.27 nje ya mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya Serikali kinyume na waraka wa Hazina namba tatu wa mwaka 2017.
Kuhusu Kampuni ya Ndege Nchini – ATCL, CAG Kichere amesema kwa mwaka wa fedha 2022/23 ilipata hasara ya TZS bilioni 56.64, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 61 kutoka hasara ya Bil. 35.24 iliyoripotiwa mwaka uliopita.
“Ukaguzi wa ripoti ya kubadilisha mita za umeme za TANESCO kwa mwaka wa fedha 2022/23 ulibaini kuwa mita 108,088 kati ya mita 602,269 zilibadilishwa na TANESCO kabla ya kipindi cha uhai wa matumizi yake kuisha. Katika mita hizo, mita 13,493 zilibadishwa ndani ya mwaka mmoja baada ya kufungwa na mita 94,595 zilikuwa na muda mfupi wa matumizi kati ya mwaka mmoja hadi miaka 15 kinyume na muda unaokubalika wa miaka 20,” alisema Kichere.
Hata hivyo katika ukaguzi wake pia CAG mesema “Mashirika nane ya umma yalikusanya mapato ya Shilingi Bil. 23.27 nje ya mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya Serikali kinyume na waraka wa Hazina namba tatu wa mwaka 2017.”