Kada wa CCM Yusuf Kazi aonyesha kukerwa na TUKIO la gari aina ya Land Cruiser V8 lenye namba nambari za usajili T 774 BDL likiwa na bendera ya CCM kukamatwa likiwa limebeba wahamiaji haramu 20 kutoka nchi ya Ethiopia huko mkoani Manyara amesema nikukichafua Chama awataka jeshi la Uhamiaji wachukue hatua ili wachangie mapato ya taifa.
Amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam amesema yeye akiwa ni mwanachama wa CCM na kada suala hilo limemuhudhunisha sana kwani ni suala la kukidhalilisha CCM kwani inawezekana kuwa muhusika wa tukio sio kiongozi wala mwanachama wa CCM.
“Inawezekana nia yake ilikuwa kuchafua CCM na Mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inawezekana Ile ikiwa ni gari tu la mtu ameamua kuweka bendera ya CCM ambaye ni mharifu kama walivyowaallrifu wengine akawa anachafus Chama chetu.”
“Lakini tunaona kila wakati kumekuwa na Matukio ya kukamatwa hawa wahamiaji haramu ambao wanakuwa wanapita wakitokea nchi jirani ya Kenya wakielekea Msumbiji, Malawi, Zambia mpaka Afrika Kusini hawakai hapa nchini wao wanakuwa wakisafiri kwenda Afrika Kusini”
“Mimi kwa hesabu za haraka haraka naona kuna jambo serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani na jeshi la Uhamiaji inatakiwa ifanye kitu kwani watu hawa kwani magerezani tumekuwa na wafungwa wengi sana wa Matukio hayo na takwimu zinaonyesha wahamiaji hao wanafikia elfu 20 kwa mwaka tunawakamata.”
Amesema, “Watu elfu 20 ni wengi sana ambao wanakaa ndani ya magereza yetu natunapata jukumu kubwa ambalo serikali inatumia fedha nyingi kuwalisha hawa watu bila ya kuwa na sababu za msingi.”
“Hawa watu wakikamatwa wanapelekwa mahakamani wanafungwa kifungo kisichozidi miezi sita baada ya hapo hubaki gerezani Ndugu zao hawaji kuwachukua wanaendelea kula na kuhudumiwa na serikali yetu”
“Na kila mtu akilkaa gerezani au mahabusu huigharimu serikali shillingi 500/- kwa siku ukizidisha mara siku 366 za mwaka utapata gharama serikali inaingia kwa kumlisha mtu huyo kwa mwaka ukizidisha mara idadi ya wahamiaji haramu wanaokamatwa nchini utaona jinsi serikali inavyoingia gharama kubwa isiyona sababu”
“Suala la kujiuliza ni kwamba wanapitaje huko kwenye mataifa mengine yaani inaonekana hapa kwetu kuna udhaifu kidogo, lakini kwanini tusiwatengenezee transite Visa walipie kwa kuwatengenezea utaratibu mzuri waendelee na safari yao bila kuingia gharama za nchi zingine.”
“Tunachofanya ni kulitia taifa hasara na tunazuia safari za watu na tunafanyq kazi za nchi zingine kwa kuzuia watu wanaoenda huko”
“Najua Kamishina generally wetu wa Uhamiaji anafanya kazi kubwa na nzuri na anapambana sana katika hilo jeshi lakini maoni yangu ni hayo yaani tukichukua Dola 100 kwa kila mmoja kuanzia katika mipaka yetu ya Namanga, Holoholo na sehemu zingine wakaangalie utaratibu ambao utasaidia kuvuka kwa transite Visa wakaenda zao”
“Itatuwezesha sisi kupunguzia serikali gharama za kuwatunza hawa wahamiaji haramu na pili tutaongeza mapato ya nchi kwani tukichukua hiyo Dola 100 kwa kila mmoja mara mwaka tutapata faida sana badala ya kuendelea serikali kugharamika”
“Wanamaliza kifungo na Ndugu zao hawaji kuwachukua wanaendelea kula na kuhudumiwa wakiwa sio wajibu wetu” amesema Yusuf.
Aidha ameitaka Wizara ya Mambo ya ndani kuangalia kwa upya Sheria zake kumaliza hili na wahamiaji wanaokuja kihalali nchini tuwapokee na wanaopita tuwaache wapite zao.
Hata hivyo amekumbusha maazimio ya kamati ya kusukuma mashauri ya kesi za jinai nchini iliwahi kutoa ushauri hivyo maelekezo yake yatekelezwe kwa kufanyia kazi.
“Kwanini yale mapendekezo yao hayafanyiwi kazi mpaka CCM tunadhalilika namna hii?” Alihoji Kada wa CCM Yusuf.