Maafisa wa usalama wa Taliban katika eneo la kusini mashariki mwa Afghanistan wamesema bomu la kutegwa ardhini lililipuka usiku na kuua watoto tisa.

Bomu hilo, linadaiwa halikulipuka awali wakati wa mizozo ya zamani na lililipuka Machi 31  wakati kikundi cha watoto walipokuwa wakilichezea katika Wilaya ya Geru, iliyopo jimbo la Ghazni.

Msemaji wa Serikali, Hamidullah Nisar alidai kuwa bomu hilo liliachwa wakati wa uvamizi wa Russia nchini Afghanistan katika miaka ya 1980.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa mjini Kabul ulisema maelfu ya raia, wakiwemo wanawake na watoto, nchini Afghanistan waliuawa au kujeruhiwa na mabomu ya kutegwa ardhini na vilipuzi vingine vilivyobakia baada ya vita.

Aziz Ki mchezaji bora Ligi Kuu
MALIMWENGU: Mapepe yalivyoniingiza matatani